Skip to content
آل عِمران /

Aya 164

3 : 164

Aya 164 of آل عِمران (3 : 164). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 164

لَقَدۡ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذۡ بَعَثَ فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡ أَنفُسِهِمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ

Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu amewafadhili Waumini wale wa mwanzo walio kuwa na Nabii s.a.w. kwa kuwapelekea Mtume aliye tokana na wao wenyewe, akiwasomea Aya za Kitabu, na akiwat'ahirisha na itikadi mbovu, akiwafundisha Qur'ani na Sunna za Mtume, na ilhali kabla ya kuletwa Mtume, walikuwa katika ujinga na ubabaishi na upotovu.