Skip to content
آل عِمران /

Aya 105

3 : 105

Aya 105 of آل عِمران (3 : 105). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 105

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ تَفَرَّقُواْ وَٱخۡتَلَفُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Wala msiwe kwa kupuuza kwenu kuamrisha mema na kukataza maovu--mambo ambayo ndiyo yanayo kukusanyeni katika kheri na Dini ya Haki--kama wale walio puuza kuamrisha mema na kukataza maovu,wakagawika mapande mbali mbali, wakakhitalifiana katika Dini yao baada ya kuwafikilia hoja zilizo wazi, zenye kubainisha Haki. Na hao walio farikiana wakakhitalifiana, watapata adhabu kuu.