Skip to content
آل عِمران /

Aya 30

3 : 30

Aya 30 of آل عِمران (3 : 30). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 30

يَوۡمَ تَجِدُ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ مِنۡ خَيۡرٖ مُّحۡضَرٗا وَمَا عَمِلَتۡ مِن سُوٓءٖ تَوَدُّ لَوۡ أَنَّ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَهُۥٓ أَمَدَۢا بَعِيدٗاۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَٱللَّهُ رَءُوفُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyo yafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya ilio ufanya. Itapenda nafsi lau kungekuwako masafa marefu baina ya ubaya huo na yeye. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.

Explanation & meanings · 1
  1. Basi na watahadhari wale wanao ikhalifu amri yake na Siku ambayo kila mtu atakuta vitendo vyake vya kheri hata kilicho kichache kimeletwa hadharani; na pia uovu wake alio utenda ambao angetamani lau kuwa uko mbali, mwisho wa umbali, hata asiuone kwa kuuchukia na kukhofu kutumbukia katika adhabu zake. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni na adhabu zake pindi mkitokana na ulinzi wake na utawala wake, ambao ni upole na rehema kwa waja wake.