Skip to content
آل عِمران /

Aya 69

3 : 69

Aya 69 of آل عِمران (3 : 69). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 69

وَدَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يُضِلُّونَكُمۡ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao penda kukupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao, nao wenyewe hawatambui.

Explanation & meanings · 1
  1. Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu wanao tamani kuwapotoa Waumini na kuwafitini waache Dini yao, kwa kuwatilia mikorogo ya kudhoofisha itikadi. Lakini katika kazi yao hii hawatampotoa mtu ila nafsi zao wenyewe kwa kuendelea katika upotovu, ambao utakuja kuwagubika wao wenyewe tu, na wala hawajui kuwa matokeo ya juhudi yao ovu yatawapata wenyewe, wala hayatawadhuru Waumini.