Skip to content
Al-'Imran /

Aya 191

3 : 191

Aya 191 of Al-'Imran (3 : 191). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-'Imran Aya 200
Sura · Al-'Imran
Kiswahili · Barawani
3 : 191

ٱلَّذِينَ يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمۡ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ رَبَّنَا مَا خَلَقۡتَ هَٰذَا بَٰطِلٗا سُبۡحَٰنَكَ فَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa Mbingu na Ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.

Explanation & meanings · 1
  1. Ni shani ya wenye akili kuwa kila pahali wao wanahudhurisha katika nafsi zao adhama na utukufu wa Mwenyezi Mungu, wakiwa wamesimama au wamekaa au wamejinyoosha kitandani, na wanazingatia uumbaji wa mbingu na ardhi pamoja na viliomo ndani yake, na huku wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuumba haya ila kwa hikima uliyo ikadiria. Na Wewe umetakasika na kila upungufu. Bali umeumba hivi vyote kuwa ni dalili ya kudra yako, na ishara ya upeo wa hikima yako. Utuhifadhi na adhabu ya Moto kwa kutuwezesha kukut'ii.