Skip to content
Orodha ya Sura /

الأعرَاف

الأعرَاف is chapter 7 of the Quran and has 206 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

206 Aya Sura Na. 7
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

الٓمٓصٓ

ALIF LAM MYM 'SAAD .

Explanation & meanings · 1
  1. Alif Lam Mym 'Saad. (A.L.M.S'.) Hizi ni harufi za kutamkwa ambazo zinaanzia baadhi ya Sura za Makka, kwa ajili ya kuwazindua Washirikina kuwa hakika hii Qur'ani Tukufu imeundwa kwa harufi zile zile wanazo zitamka wao. Na juu ya hivyo wao wanaemewa hawawezi kuleta mfano wake. Kadhaalika harufi hizi zinapo somwa huwazindua wao wasikilize, kwa kuwa walikuwa wananasihiwa na wakubwa zao kuwa wasiisikilize Qur'ani.

كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Kitabu kilicho teremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini.

Explanation & meanings · 1
  1. (Ewe Nabii!) Umeteremshiwa wewe Qur'ani ili uwaonye hao wanao kanya wapate kuamini, na uwakumbushe Waumini wapate kuzidi Imani yao. Basi usiingie dhiki katika kifua chako unapo ifikilisha kwa kukhofu kuwa utakanushwa.

ٱتَّبِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ وَلَا تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۗ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka.

Explanation & meanings · 1
  1. (Enyi Watu!) Fuateni aliyo kufunulieni Mola wenu Mlezi, wala msiwafuate marafiki au walinzi wengineo badala yake Yeye, mkawa mnawaitikia wao na mkiwaomba msaada! Itakuwa kama hamkuwaidhika ikiwa mtaiacha Dini ya Mwenyezi Mungu na muifuate nyengineyo, hali ya kuwa yapo mengi ya kuzingatia katika haya mliyo funuliwa.

وَكَم مِّن قَرۡيَةٍ أَهۡلَكۡنَٰهَا فَجَآءَهَا بَأۡسُنَا بَيَٰتًا أَوۡ هُمۡ قَآئِلُونَ

Na miji mingapi tuliiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipo kuwa wamelala adhuhuri.

Explanation & meanings · 1
  1. Kwani Sisi tumekwisha iteketeza miji kadhaa wa kadhaa, kwa sababu watu wao walikuwa wakiwaabudu wasio kuwa Mwenyezi Mungu, na kwa kuwa katika mwendo wao hawakufuata Njia yake. Ikawajia adhabu yetu wakati wao wameghafilika na wametuwa usiku nao wamelala, kama yalivyo wapata kaumu ya Lut'; au wakatekezwa mchana nao wamepumzika wakati wa kujinyoosha, kama yalivyo wapata kaumu ya Shua'ib.

فَمَا كَانَ دَعۡوَىٰهُمۡ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَآ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Basi hakikuwa kilio chao ilipo wafikia adhabu yetu, isipo kuwa kusema: Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.

Explanation & meanings · 1
  1. Basi wakaungama kwa madhambi yao yaliyo waletea msiba wao. Hakuwa hata mmoja katika wao walipo ona adhabu ila alisema, na wakati huo kusema huko hakufai kitu: Hakika sisi tulikuwa tumejidhulumu nafsi zetu kwa maasiya, wala Mwenyezi Mungu hakutudhulumu kwa kutupa adhabu.