7 : 109
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi.
Explanation & meanings · 1
- Musa alipo ionyesha Ishara ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, zilitibuka roho za wapambe wa Firauni na waheshimiwa wa kaumu yake, wakasema katika kujipendekeza kwa Firauni na kumtetea: Hakika huyu ni bingwa katika ilimu ya uchawi, wala hii si Ishara itokayo kwa Mwenyezi Mungu!!