Skip to content
الأعرَاف /

Aya 90

7 : 90

Aya 90 of الأعرَاف (7 : 90). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 90

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَئِنِ ٱتَّبَعۡتُمۡ شُعَيۡبًا إِنَّكُمۡ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ

Na waheshimiwa walio kufuru katika kaumu yake wakasema: Mkimfuata Shua'ib, basi hakika hapo nyinyi mtakuwa mlio khasiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Hapo basi wale watu walikata tamaa ya kuwafanya Shua'ib na walio kuwa naye wawafuate wao. Na wakajua kuwa hakika hao walikuwa wamethibiti katika Dini yao. Kadhaalika waliogopa wasizidi kuwa wengi wale walio hidika pamoja na Shua'ib kwa kudhihiri nguvu zake na kuthibiti kwake juu ya wito wake. Kwa hivyo wale waheshimiwa wa kikafiri wakawaelekea wafwasi wao wakiwatisha kwa kusema: Wallahi! Mkimfuata Shua'ib mkakubali wito wake, basi hapana shaka nyinyi utakutokeni utukufu wenu na utajiri wenu kwa kufuata dini potovu wasio kuwa wakiifuata wazee wenu.