Skip to content
الأعرَاف /

Aya 93

7 : 93

Aya 93 of الأعرَاف (7 : 93). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 93

فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡۖ فَكَيۡفَ ءَاسَىٰ عَلَىٰ قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ

Basi akawaachilia mbali na akasema: Enyi kaumu yangu! Nimekufikishieni Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na nimekunasihini; basi vipi niwahuzunikie watu makafiri?

Explanation & meanings · 1
  1. Shua'ib alipo ona hilaki ya kuvuruga iliyo wateremkia wale watu, basi aliwaachilia mbali, na akasema kujivua nafsi yake asiwe mkosa pamoja nao: Mimi nimekufikishieni ujumbe wa Mola wenu Mlezi unao pelekea mpate wema nyinyi, lau kuwa mngeli ufuata. Na mimi nimefanya ukomo wa uwezo wangu katika kukunasihini, na kukuwaidhini kwa mambo ya kukuokoeni na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Basi vipi tena niwasikitikie mno watu makafiri? Hayawi hayo baada ya kuwa mimi nimekwisha jiudhuru kwao, na nikatumia juhudi yangu kwa ajili ya kutaka kuwahidi na kuwaokoa, na wao wakakhiari kufuata yale yale ya kuwahiliki.