Skip to content
الأعرَاف /

Aya 75

7 : 75

Aya 75 of الأعرَاف (7 : 75). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 75

قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لِلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِمَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُمۡ أَتَعۡلَمُونَ أَنَّ صَٰلِحٗا مُّرۡسَلٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قَالُوٓاْ إِنَّا بِمَآ أُرۡسِلَ بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ

Waheshimiwa wa kaumu yake wanao jivuna waliwaambia wanao onewa wenye kuamini miongoni mwao: Je, mnaitakidi ya kwamba Swaleh ametumwa na Mola Mlezi wake? Wakasema: Hakika sisi tunayaamini yale aliyo tumwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Wale wenye kiburi katika watu wa mbele-mbele na uwongozi waliwasemeza wanyonge kwa kuwalaumu na kuwadhalilisha: Hivyo nyinyi mnaitakidi kuwa kweli Swaleh ametumwa na Mola Mlezi wake? Watu wa Haki wakawajibu: Sisi tunaitakidi na tunakubali aliyo tumwa kwetu.