Skip to content
الأعرَاف /

Aya 116

7 : 116

Aya 116 of الأعرَاف (7 : 116). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 116

قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ

Akasema: Tupeni! Basi walipo tupa waliyazuga macho ya watu na wakawatia khofu, na wakaleta uchawi mkubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Musa akwajibu jawabu ya mwenye imani ya kushinda, akionyesha kutowabali: Tupeni nyinyi kwanza hicho mnacho tupa. Walipo tupa kila mmoja wao, navyo ni kamba na fimbo, macho ya watu yalizugwa, na ikawapitikia kuwa walicho kifanya kile ni hakika kweli. Na hali haikuwa ila ni kiini macho tu. Mambo yale yaliwatisha watu, na nyoyo zao zikaingia khofu na kitisho. Kwani wachawi wale waliwaletea watu uchawi unao onekana ni mkubwa, na athari yake katika macho yao ni kubwa!