Skip to content
الأعرَاف /

Aya 26

7 : 26

Aya 26 of الأعرَاف (7 : 26). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 26

يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ قَدۡ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمۡ لِبَاسٗا يُوَٰرِي سَوۡءَٰتِكُمۡ وَرِيشٗاۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقۡوَىٰ ذَٰلِكَ خَيۡرٞۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ

Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamngu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu mpate kukumbuka.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi Binaadamu! Sisi tumekuneemesheni. Tumekuumbieni nguo kusitiri tupu zenu, na vitu vya pambo. Lakini ut'iifu ndio nguo bora ya kukukingeni na adhabu. Neema hizo ni katika Ishara zenye kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu, na rehema yake, ili watu waukumbuke utukufu wake. Yeye tu ndiye anaye stahiki Ungu. Na kisa hichi ni katika nyendo za Mwenyezi Mungu za uumbaji wake, zinazo bainisha nini malipo ya kuvunja amri ya Mwenyezi Mungu, ili watu wakumbuke, na wafanye pupa kumt'ii Allah na kumshukuru.