Skip to content
الأعرَاف /

Aya 145

7 : 145

Aya 145 of الأعرَاف (7 : 145). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 145

وَكَتَبۡنَا لَهُۥ فِي ٱلۡأَلۡوَاحِ مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡعِظَةٗ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ فَخُذۡهَا بِقُوَّةٖ وَأۡمُرۡ قَوۡمَكَ يَأۡخُذُواْ بِأَحۡسَنِهَاۚ سَأُوْرِيكُمۡ دَارَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonyesheni makaazi ya wapotofu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na tulimbainishia Musa katika zile mbao za Taurati kila kitu kilicho khusu mawaidha na hukumu zilizo elezwa mbali mbali, wanazo hitajia watu duniani na Akhera. Na tukamwambia: Zishike hizi mbao baraabara na kwa kuazimia. Na waamrishe watu wako washike yaliyo bora humo, kama kusamehe badala ya kulipiza kisasi, na kuachilia badala ya kungojea, na kulegeza badala ya kukaza. Enyi kaumu ya Musa! Nitakuonyesheni katika vitabu vyenu makaazi ya wale wanao asi amri za Mwenyezi Mungu, na watavyo angamia, ili mpate kuzingatia. Basi msende kinyume yakakusibuni yalio wasibu hao waasi.