Skip to content
الأعرَاف /

Aya 128

7 : 128

Aya 128 of الأعرَاف (7 : 128). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 128

قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ

Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hapo Musa aliona kama dalili za huzuni katika watu wake, basi akawatia nguvu katika azma yao. Akawambia: Mtakeni Mwenyezi Mungu msaada na kukuungeni mkono. Na kuweni imara, wala msifazaike. Kwani ardhi yote imo katika nguvu za uwezo wa Mwenyezi Mungu na ufalme wake. Humrithisha amtakaye katika waja wake, wala si ya Firauni. Na mwisho mwema wataupata wale wanao mcha Mwenyezi Mungu kwa kushikamana naye na kuzikamata hukumu zake.