7 : 201
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ إِذَا مَسَّهُمۡ طَٰٓئِفٞ مِّنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ تَذَكَّرُواْ فَإِذَا هُم مُّبۡصِرُونَ
Hakika wale wamchaomungu zinapowagusa pepesi za Shetani, mara huzindukana na hapo huwa niwenye kuiyona haki
Explanation & meanings · 1
- Hakika wale wamchao Mola wao Mlezi, na wakaweka baina yao na maasi kinga cha kuzuia uchochezi wa Shetani unao wapitia kuwaachisha yaliyo waajibu wao, hukumbuka uadui wa Shetani na vitimbi vyake. Kwa hivyo hao wanaiona Haki, basi ndio wanarejea.