7 : 203
وَإِذَا لَمۡ تَأۡتِهِم بِـَٔايَةٖ قَالُواْ لَوۡلَا ٱجۡتَبَيۡتَهَاۚ قُلۡ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ مِن رَّبِّيۚ هَٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Na usipo waletea Ishara waitakayo husema: Kwa nini hukuibuni? Sema: mimi ninafuata yanayo funuliwa kwangu kutokana na Mola Mlezi wangu. Hii (Qur'ani) ni hoja zinazo toka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu na rehema kwa watu wanao amini.
Explanation & meanings · 1
- Na usipo waletea makafiri Ishara wanayo itaka kwa inadi na ukafiri, husema: Kwa nini hukuitaka? (au hukuizua? Makusudio yao ni kuwa Mtume s.a.w. akizibuni Aya zote.) Waambie: Mimi sifuati ila Qur'ani ninayo funuliwa kwa wahyi kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na waambie: Hii Qur'ani ni hoja zinazo toka kwa Mola Mlezi wenu kukuonyesheni njia za Haki. Nayo ina uwongofu, na rehema, kwa Waumini, kwa sababu wao wanaifuata kwa vitendo.