Skip to content
الأعرَاف /

Aya 185

7 : 185

Aya 185 of الأعرَاف (7 : 185). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 185

أَوَلَمۡ يَنظُرُواْ فِي مَلَكُوتِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ وَأَنۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَدِ ٱقۡتَرَبَ أَجَلُهُمۡۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ

Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vitu alivyo viumba Mwenyezi Mungu, na pengine ajali yao imekwisha karibia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?.

Explanation & meanings · 1
  1. Wamemwambia Muhammad mwongo kwa Tawhidi anayo waitia, wala hawakutazama kwa kuzingatia na kutafuta dalili za ufalme mtukufu wa Mwenyezi Mungu ulioko katika mbingu na ardhi na viliomo ndani yao, zinazo onyesha ukamilifu wa uwezo wa huyu Mwenye kuunda, na zinazo onyesha Umoja wake wa pekee. Wala hawakufikiri kuwa ajali yao imekwisha karibia, au huenda ikawa imekaribia, wapate kufanya haraka kutupia nadhari na kuitafuta Haki kabla ya kuzuka ajali. Ikiwa basi watu hawa hawaamini maneno ya Qur'ani watakuja amini maneno gani baada yake