Skip to content
الأعرَاف /

Aya 94

7 : 94

Aya 94 of الأعرَاف (7 : 94). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 94

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّآ أَخَذۡنَآ أَهۡلَهَا بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَضَّرَّعُونَ

Na hatukumtuma Nabii yeyote katika mji ila tuliwapatiliza wakaazi wake kwa taabu na mashaka ili wapate kunyenyekea.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Sisi hatukumpeleka Nabii yeyote kwenye mji akawalingania watu wake wafuate Dini ya Mwenyezi Mungu iliyo sawa, na wao wakakataa kuukubali huo wito, ila tuliwapatiliza kwa ufakiri na maradhi, ili wapate kuwa wanyonge na wamwombe Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, na kumsafia niya wapate kuondokewa na balaa na wamuitikie Mtume wake.