7 : 80
وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!
Explanation & meanings · 1
- Na hakika tulimtuma Nabii wa Mwenyezi Mungu, Lut', kwa kaumu yake; awaite wafuate Tawhidi, yaani ibada ya Mwenyezi Mungu mmoja. Na awazindue juu ya waajibu wa kuachana na makosa maovu kabisa waliyo kuwa wakiyafanya. Aliwaambia: Nyinyi mnakwenda kufanya jambo lilio pita mpaka kwa ubaya wake, kinyume na maumbile? Mmezua uchafu huo ambao unapingana na khulka, na ambao hapana watu walio kutangulieni walio fanya hayo!