Skip to content
الأعرَاف /

Aya 134

7 : 134

Aya 134 of الأعرَاف (7 : 134). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 134

وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ

Na ilipo waangukia adhabu wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa aliyo kuahidi. Ukituondolea adhabu hii hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili wende nawe.

Explanation & meanings · 1
  1. Katika kuzidi kigeugeu chao kama zinavyo badilika sababu, walikuwa kila ikiwashukia namna yoyote ya adhabu wakisema kwa shida na machungu yanayo wapata: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola Mlezi wako, kwa vile alivyo kuahidi kuwa ukimwomba atakupa miujiza na atakuitikia dua, atuondolee adhabu hii. Na sisi tunakuapia kuwa ukituondolea basi bila ya shaka tutakuitikia na tutawaachilia wende nawe Wana wa Israili kama ulivyo taka!