Skip to content
الأعرَاف /

Aya 92

7 : 92

Aya 92 of الأعرَاف (7 : 92). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأعرَاف Aya 206
Sura · الأعرَاف
Kiswahili · Barawani
7 : 92

ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَاۚ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَانُواْ هُمُ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Wale walio mkanusha Shua'ib wakawa kama kwamba hawakuwako. Walio mkanusha Shua'ib ndio walio kuwa wenye kukhasiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Hii ndio shani ya Mwenyezi Mungu na hao walio mkanusha Shua'ib, na wakamtishia, na wakamwonya kuwa watamfukuza katika mji wao, na wakafanya kila kitu kuupinga wito wake. Wamehiliki wao na ukahiliki mji wao, ikawa kama kwamba humo hawakuwahi kuishi wale walio mkadhibisha Shua'ib na wakadai kuwa ati atakaye mfuata atakuwa amekhasiri, na wakatilia nguvu madai hayo. Na lililo kuwa ni kuwa wao ndio walio poteza neema yao ya dunia na Akhera.