Skip to content
Orodha ya Sura /

يُوسُف

يُوسُف is chapter 12 of the Quran and has 111 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

111 Aya Sura Na. 12
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.

Explanation & meanings · 1
  1. Alif, Lam, Raa. Hizi harufi na mfano wake, zinazo fanya maneno yenu, enyi Waarabu, ndizo hizo hizo zinazo fanya Aya za hichi Kitabu, ambacho ni muujiza unao waemea watu kuuiga. Muujiza ulio wazi unao fafanua kwa kila mwenye kutafuta uwongozi ndani yake, na uwongofu. Na kwa hizi harufi za kutamkika zikasikilizana sauti yake wanazinduliwa watu watanabahi. Basi wasikilize, ijapo kuwa waliwafikiana kuwa wasisikilize.

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Sisi tumemteremshia Mtume wetu haya maneno kwa lugha yenu ya Kiarabu yasomwe na yahifadhiwe, ili muyafahamu, na muwafikishie watu wote.

نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ

Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na ijapo kuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio jua.

Explanation & meanings · 1
  1. Sisi tunakusimulia, ewe Nabii, visa vizuri kabisa kwa kukufunulia Kitabu hichi. Na kabla ya haya ulikuwa umeghafilika nayo, huyajui, haya, wala mawaidha yaliomo ndani yake, na Aya zake zilizo wazi.

إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ إِنِّي رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُهُمۡ لِي سَٰجِدِينَ

Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia.

Explanation & meanings · 1
  1. Katika visa hivi, ewe Nabii, kipo hichi kisa cha Yusuf, pale alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeona usingizini nyota hidaa'shara, (kumi na moja) na jua, na mwezi. Nimeona vyote hivyo vikininyenyekea, vikisujudu mbele yangu. Yusuf, Alayhi Ssalam, alikuwa mwana wa Yaaqub, Muabrani, Mkanaani. Akauzwa Misri katika enzi ya utawala wa wavamizi wa kigeni waitwao Wahiksos. Na kwa ionekanavyo hao Wahiksos ni katika kabila za Kisami walio ingia Misri kutoka Sham wakaiteka Delta ya Misri mnamo mwaka 1730 k.k. ( kabla ya Nabii Isa a.s.) na kabla ya kumalizika enzi ya ukoo wa kumi na tatu wa Mafirauni. Wakaihukumu Misri kwa muda wa karne unusu. Wakafukuzwa mnamo mwaka 1580 k.k. na Ahmas wa Mwanzo aliye anzisha ukoo wa 18. Wakatolewa nje ya mipaka ya Misri.

قَالَ يَٰبُنَيَّ لَا تَقۡصُصۡ رُءۡيَاكَ عَلَىٰٓ إِخۡوَتِكَ فَيَكِيدُواْ لَكَ كَيۡدًاۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.

Explanation & meanings · 1
  1. Baba yake akamwambia: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako hii. Itakuja watia husda katika nyoyo zao, na Shetani atawachochea wazue njama kukupinga. Watakuja kufanyia hila na vitimbi! Hakika Shetani ni adui wazi wa binaadamu!