Skip to content
يُوسُف /

Aya 51

12 : 51

Aya 51 of يُوسُف (12 : 51). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 51

قَالَ مَا خَطۡبُكُنَّ إِذۡ رَٰوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفۡسِهِۦۚ قُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا عَلِمۡنَا عَلَيۡهِ مِن سُوٓءٖۚ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡـَٰٔنَ حَصۡحَصَ ٱلۡحَقُّ أَنَا۠ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipo mtaka Yusuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliye mtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli.

Explanation & meanings · 1
  1. Mfalme akawakusanya wale wanawake, na akawauliza: Ilikuwa vipi hali yenu pale mlipo jaribu kumkhadaa Yusuf aghafilike na wema wake na usafi wa nafsi yake? Je, mlimwona amemili kwenu? Wakamjibu: Mwenyezi Mungu ametakasika! Hakumsahau mja wake hata uchafuke usafi wake. Sisi hatukuona kwake lolote la kumtia dosari. Hapo basi wema ukapata nguvu katika moyo wa Zuleikha (mke wa Mheshimiwa) akaingia kusema: Sasa kweli imedhihiri! Ni mimi ndiye niliye mkhadaa, na nikajaribu kumzaini kinyume na nafsi yake kwa kumghuri. Lakini yeye alishikilia usafi wake! Na sasa nahakikisha kuwa yeye ni katika watu wa kweli. Na ni haki tupu alipo nirudishia tuhuma mimi na kunitia makosani!