Skip to content
يُوسُف /

Aya 41

12 : 41
يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 41

يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسۡقِي رَبَّهُۥ خَمۡرٗاۖ وَأَمَّا ٱلۡأٓخَرُ فَيُصۡلَبُ فَتَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِن رَّأۡسِهِۦۚ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ٱلَّذِي فِيهِ تَسۡتَفۡتِيَانِ

Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watamla kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilo kuwa mkiuliza.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi wenzangu wawili wa gerezani! Hii basi ndiyo tafsiri ya ndoto zenu: Ama mmoja wenu aliye kamua zabibu katika ndoto yake, atatoka jela, na atakuwa akimnywesha mvinyo Mfalme. Na ama huyu wa pili atatundikwa msalabani, na ataachwa msalabani ndege wakimla kichwa chake. Yamekwisha timia hayo mambo kama nilivyo eleza kwa mujibu mlivyo nitaka nieleze tafsiri ya hizo ndoto!