Skip to content
Yusuf /

Aya 85

12 : 85

Aya 85 of Yusuf (12 : 85). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Yusuf Aya 111
Sura · Yusuf
Kiswahili · Barawani
12 : 85

قَالُواْ تَٱللَّهِ تَفۡتَؤُاْ تَذۡكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوۡ تَكُونَ مِنَ ٱلۡهَٰلِكِينَ

Wakasema: Wallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe katika walio hiliki.

Explanation & meanings · 1
  1. Siku zikapita na Yaa'qub kazama katika majonzi yake. Wanawe wakaogopa isije kuwa khatari. Wakamkabili kumtaka apunguze huzuni yake, nao wako baina ya kumwonea huruma na kuchukia kuwa bado yu ngali akimkumbuka Yusuf wakamwambia: Kama hukujipunguzia nafsi yako hapana shaka kumkumbuka Yusuf kutakuzidishia machungu yako yakukondeshe mpaka ukaribie kufa, au ufe khasa!