Skip to content
يُوسُف /

Aya 58

12 : 58

Aya 58 of يُوسُف (12 : 58). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 58

وَجَآءَ إِخۡوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَعَرَفَهُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ

Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia kwake. Yeye akawajua na wao hawakumjua.

Explanation & meanings · 1
  1. Ukame ukazidi kushtadi katika nchi jirani na Misri. Ikawapata watu wa Yaa'qub shida vile vile kama ilivyo wapata wengineo. Watu walikwenda Misri kutoka kila pande baada ya kujua matengenezo ya Yusuf ya kuweka akiba chakula, na kujitayarisha kwake kwa miaka ya ukame. Yaa'qub aliwatuma wanawe wende kutafuta chakula, lakini akabaki naye nduguye Yusuf kwa mama kwa kumkhofia. Wale watoto wake walipo fika Misri wakenda moja kwa moja kwa Yusuf, naye akawatambua, lakini wao hawakumjua.