Skip to content
يُوسُف /

Aya 56

12 : 56
يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 56

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi namna hivi tukampa Yusuf cheo katika nchi; anakaa humo popote anapo penda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupuuzi malipo ya wafanyao mema.

Explanation & meanings · 1
  1. Mfalme alilikubali ombi lake, akamfanya waziri wake. Hivyo basi Mwenyezi Mungu alimneemesha Yusuf kwa neema nzuri, akampa madaraka na uwezo katika nchi ya Misri, akienda humo atakapo. Na hii ndiyo shani yake Mwenyezi Mungu kwa waja wake, humpa neema yake amtakaye katika wao, wala hawanyimi thawabu zao, bali huwapa ujira wao wa wema wautendao kwa kuwalipa mema hapa hapa duniani.