Skip to content
يُوسُف /

Aya 93

12 : 93

Aya 93 of يُوسُف (12 : 93). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 93

ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِي يَأۡتِ بَصِيرٗا وَأۡتُونِي بِأَهۡلِكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mje nao watu wenu wote wa nyumbani.

Explanation & meanings · 1
  1. Kisha Yusuf akawauliza khabari za baba yao. Walipo mwambia kuwa hali yake ni mbaya na hawezi kuona kwa wingi wa hamu na majonzi, aliwapa kanzu yake, na akawaambia: Rejeeni kwa baba yangu, na hii kanzu mwekeeni usoni pake. Kwa hivyo atakuwa na yakini kuwa mimi nimo katika salama, na moyo wake utajaa furaha, na Mwenyezi Mungu atamjaalia iwe ni sababa ya kurejea kuona kwake. Hapo tena njooni naye kwangu, na ahali zenu wote pamoja.