Skip to content
يُوسُف /

Aya 33

12 : 33

Aya 33 of يُوسُف (12 : 33). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 33

قَالَ رَبِّ ٱلسِّجۡنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدۡعُونَنِيٓ إِلَيۡهِۖ وَإِلَّا تَصۡرِفۡ عَنِّي كَيۡدَهُنَّ أَصۡبُ إِلَيۡهِنَّ وَأَكُن مِّنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ

Yusuf akasema: Ee Mola Mlezi wangu! Nastahabu kifungo kuliko haya anayo niitia. Na usipo niondoshea vitimbi vya wanawake mimi nitamili kwao, na nitakuwa katika wajinga.

Explanation & meanings · 1
  1. Yusuf akasema naye alisikia vile vitishio, na akasikia kwa wale wanawake nasiha ya kuwa amkubalie, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nakhiari kifungo kuliko hayo anayo nitakia huyu mwanamke. Kwani hayo ni kukuasi Wewe. Na kama Wewe hunikingi na shari ya vitimbi vyao na hila zao nitakuja wakubalia, na nitakuwa miongoni mwa wajinga walio potea.