12 : 28
فَلَمَّا رَءَا قَمِيصَهُۥ قُدَّ مِن دُبُرٖ قَالَ إِنَّهُۥ مِن كَيۡدِكُنَّۖ إِنَّ كَيۡدَكُنَّ عَظِيمٞ
Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Bila ya shaka vitimbi vyenu ni vikuu.
Explanation & meanings · 1
- Mume alipoona kuwa kanzu ya Yusuf imechanwa mgongoni alimwambia mkewe: Huku kumtuhumu kwako kijana kwa yaliyo tokea na hali yeye hana makosa, ni katika vitimbi vyenu, enyi wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu mno!