Skip to content
يُوسُف /

Aya 91

12 : 91

Aya 91 of يُوسُف (12 : 91). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 91

قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ ءَاثَرَكَ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَإِن كُنَّا لَخَٰطِـِٔينَ

Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa.

Explanation & meanings · 1
  1. Wakasema: Uliyo sema ni kweli, na tunakuhakikishia kwa kiapo kwamba hapana shaka Mwenyezi Mungu amekutukuza kwa uchamngu, na subira, na sera njema. Na amekupa pia utawala na cheo cha juu. Na sisi hakika tulikuwa wenye kutenda dhambi kwa tuliyo kutendea wewe na nduguyo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu ametudhalilisha kwako, na ametulipa malipo ya wenye kutenda dhambi.