Skip to content
يُوسُف /

Aya 89

12 : 89

Aya 89 of يُوسُف (12 : 89). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 89

قَالَ هَلۡ عَلِمۡتُم مَّا فَعَلۡتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذۡ أَنتُمۡ جَٰهِلُونَ

Akasema: Je! Mmejua mliyo mfanyia Yusuf na nduguye mlipo kuwa wajinga?

Explanation & meanings · 1
  1. Yusuf akaingiwa na huruma ya udugu ambayo inasamehe maovu. Akaanza kuwafunulia khabari zake kwa kuwaambia kwa lawama: Je! Mmejua ule uovu mlio mfanyia Yusuf kwa kumtumbukiza kisimani, na maudhi mlio mfanyia nduguye, mkafanya hayo kwa ujinga ulio kusahaulisheni huruma na udugu?