Skip to content
يُوسُف /

Aya 108

12 : 108

Aya 108 of يُوسُف (12 : 108). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 108

قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Muhammad! Wazindue mwisho wa uwezo wako, na waonyeshe hadi ya juhudi yako, uwaambie: Huu ndio Mwendo wangu na Njia yangu. Nawaita watu wafuate Njia ya Mwenyezi Mungu. Na mimi nimethibiti katika hili jambo langu, na kadhalika anayaitia hayo kila mwenye kunifuata na akaiamini sharia yangu. Na namtakasa Mwenyezi Mungu Subhanahu na kila kisicho kuwa laiki yake. Wala mimi simshirikishi Yeye na kitu chochote.