Skip to content
يُوسُف /

Aya 32

12 : 32

Aya 32 of يُوسُف (12 : 32). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُوسُف Aya 111
Sura · يُوسُف
Kiswahili · Barawani
12 : 32

قَالَتۡ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِي لُمۡتُنَّنِي فِيهِۖ وَلَقَدۡ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ فَٱسۡتَعۡصَمَۖ وَلَئِن لَّمۡ يَفۡعَلۡ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسۡجَنَنَّ وَلَيَكُونٗا مِّنَ ٱلصَّٰغِرِينَ

Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliye nilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na akitofanya ninayo muamrisha basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio chini kabisa.

Explanation & meanings · 1
  1. Tena mke wa Mheshimiwa alisema kufuatiliza maneno yao: Huyu kijana ambaye uzuri wake umekuzugeni na ukakuemeeni hata yakatokea yaliyo tokea ndiye ambaye nyinyi mliye nilaumu kwa ajili yake! Na mimi kweli nilimtaka, na nikafanya juhudi kumghuri anikubalie, naye akajizuia na akakataa. Kama kwamba vile anavyo kataa ndio anazidi kumtia hamu yule mwanamke! Akasema mwanamke: Na mimi naapa! Kama hafanyi ninayo muamrisha atapata adhabu ya kifungo, na atakuwa katika madhalili wenye kudharauliwa!