Skip to content
Orodha ya Sura /

الأنبيَاء

الأنبيَاء is chapter 21 of the Quran and has 112 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

112 Aya Sura Na. 21
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمۡ وَهُمۡ فِي غَفۡلَةٖ مُّعۡرِضُونَ

IMEWAKARIBIA watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanapuuza.

Explanation & meanings · 1
  1. Umewakaribia washirikina wakati wao wa kuhisabiwa Siku ya Kiyama, nao hali wameghafilika na kitisho chake, wanapuuza kuiamini.

مَا يَأۡتِيهِم مِّن ذِكۡرٖ مِّن رَّبِّهِم مُّحۡدَثٍ إِلَّا ٱسۡتَمَعُوهُ وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ

Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo.

Explanation & meanings · 1
  1. Haiwajii Qur'ani kutokana na Mola wao Mlezi pale inapoteremka kuwakumbusha ya kuwanufaisha, ila wao huisikiliza na hali wao wameshughulika na mengine yasiyo na faida nao, wakicheza kama wachezavyo watoto wadogo.

لَاهِيَةٗ قُلُوبُهُمۡۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّجۡوَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ هَلۡ هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡۖ أَفَتَأۡتُونَ ٱلسِّحۡرَ وَأَنتُمۡ تُبۡصِرُونَ

Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi mnaona?

Explanation & meanings · 1
  1. Nyoyo zao zimo katika pumbao, hazizingatii, wameshikilia kuficha njama zao za kumpinga Nabii na Qur'ani, wakiambizana wenyewe kwa wenyewe: Huyu Muhammad si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Na Mtume hawi ila Malaika. Basi, je! Mnamsadiki Muhammad na mnahudhuria baraza za uchawi na hali nyinyi mnaona kuwa hakika huo ni uchawi?

قَالَ رَبِّي يَعۡلَمُ ٱلۡقَوۡلَ فِي ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Mtume, kwa kuwa Mwenyezi Mungu kamjuulisha waliyo kuwa wakiyasema kwa siri, aliwaambia: Mola wangu Mlezi anayajua yote yanayo semwa katika mbingu na katika ardhi, na Yeye ndiye anaye sikia kila linalo sikiwa; na anajua kila linalo tokea..

بَلۡ قَالُوٓاْ أَضۡغَٰثُ أَحۡلَٰمِۭ بَلِ ٱفۡتَرَىٰهُ بَلۡ هُوَ شَاعِرٞ فَلۡيَأۡتِنَا بِـَٔايَةٖ كَمَآ أُرۡسِلَ ٱلۡأَوَّلُونَ

Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.

Explanation & meanings · 1
  1. Bali wao wakasema: Hizi ni mchanganyiko wa ndoto alizo ziota (Muhammad); bali kazua tu na akamsingizia Mwenyezi Mungu kwa uwongo. Kisha wakaacha hayo na wakasema: Bali huyu ni mtunga mashairi anaziteka nafsi za wenye kumsikiliza. Kama kweli, basi na atuletee muujiza khasa wa kuonyesha ukweli wake, kama walivyo tumwa Manabii wa zamani wakitiwa nguvu kwa miujiza mbali mbali.