Skip to content
الأنبيَاء /

Aya 45

21 : 45

Aya 45 of الأنبيَاء (21 : 45). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنبيَاء Aya 112
Sura · الأنبيَاء
Kiswahili · Barawani
21 : 45

قُلۡ إِنَّمَآ أُنذِرُكُم بِٱلۡوَحۡيِۚ وَلَا يَسۡمَعُ ٱلصُّمُّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ

Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwi hawasikii wito wanapo onywa.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Sema: Sikuhadharisheni kwa maneno yanayo tokana nami. Lakini nakuhadharisheni kwa Wahyi (Ufunuo) unao tokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu ulio nijia mimi. Na huo ni wa Haki na kweli. Lakini hao kwa sababu ya kupuuza kwao kurefu kuipuuza Sauti ya Haki, Mwenyezi Mungu ameyaziba masikio yao mpaka wakawa kama viziwi. Na kiziwi hasikii Wito anapo hadharishwa na adhabu!