21 : 99
لَوۡ كَانَ هَٰٓؤُلَآءِ ءَالِهَةٗ مَّا وَرَدُوهَاۖ وَكُلّٞ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo.
Explanation & meanings · 1
- Lau kama hawa mlio waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni miungu inayo stahiki kuabudiwa, wasingeli ingia nanyi humo. Na nyote, wenye kuabudu na kuabudiwa, mtabaki Motoni, wala hamtatoka.