Skip to content
Orodha ya Sura /

طه

طه is chapter 20 of the Quran and has 135 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

135 Aya Sura Na. 20
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Rwwad
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

طه

Twa Ha!

Explanation & meanings · 1
  1. Herufi hizi "Twa Ha" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

مَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لِتَشۡقَىٰٓ

Hatukukuteremshia Qur-ani ili upate mashaka.

إِلَّا تَذۡكِرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰ

Bali ni ukumbusho kwa mwenye kunyenyekea.

تَنزِيلٗا مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلۡعُلَى

Ni uteremsho kutoka kwa aliyeumba ardhi na mbingu zilizo juu.

ٱلرَّحۡمَٰنُ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ ٱسۡتَوَىٰ

Arrahmani (Mwingi wa rehema), aliyeinuka juu ya Kiti cha Enzi.