21 : 46
وَلَئِن مَّسَّتۡهُمۡ نَفۡحَةٞ مِّنۡ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Na wanapo guswa na mpulizo mmoja tu wa adhabu itokayo kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka wao husema: Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.
Explanation & meanings · 1
- Na kuwa na yakini kuwa nao wakisibiwa hata na chembe ya adhabu ndogo wanayo ifanyia maskhara, hupiga kelele kwa khofu wakisema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa tunajidhulumu nafsi zetu, na tukiwadhulumu wenginewe, tulipo yakataa tuliyo ambiwa.