Skip to content
الأنبيَاء /

Aya 35

21 : 35

Aya 35 of الأنبيَاء (21 : 35). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنبيَاء Aya 112
Sura · الأنبيَاء
Kiswahili · Barawani
21 : 35

كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَنَبۡلُوكُم بِٱلشَّرِّ وَٱلۡخَيۡرِ فِتۡنَةٗۖ وَإِلَيۡنَا تُرۡجَعُونَ

Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Kila nafsi haina budi kuonja mauti. Na Sisi tunakufanyieni hapa duniani kama wenye kukupeni mtihani, kwa kukupeni yenye manufaa yenu na yenye madhara pia, ili abagulike mwenye kushukuru kwa kupewa kheri na kuvumilia balaa, na yule asiye na fadhila kwa neema aipatayo na anapapatika akipata misiba. Nanyi mtarejeshwa kwetu, na hapo tutakuhisabieni vitendo vyenu.