21 : 2
مَا يَأۡتِيهِم مِّن ذِكۡرٖ مِّن رَّبِّهِم مُّحۡدَثٍ إِلَّا ٱسۡتَمَعُوهُ وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ
Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo.
Explanation & meanings · 1
- Haiwajii Qur'ani kutokana na Mola wao Mlezi pale inapoteremka kuwakumbusha ya kuwanufaisha, ila wao huisikiliza na hali wao wameshughulika na mengine yasiyo na faida nao, wakicheza kama wachezavyo watoto wadogo.