Skip to content

Mwanamke amefungua katika mwezi wa Ramadhani siku saba, alikuwa akitokwa damu ya uzazi, na hakulipa siku hizi mpaka akajiwa na Ramadhani ya pili, na akazungukiwa katika Ramadhani ya pili na siku saba ambazo alikuwa ananyonyesha (hakufunga) kwa hoja alikuwa na maradhi, na imekaribia kuingia Ramdhani ya tatu, tupeni faida, Allah awalipeni thawabu.

السؤال

Swali la 1:

Mwanamke amefungua katika mwezi wa Ramadhani siku saba, alikuwa akitokwa damu ya uzazi, na hakulipa siku hizi mpaka akajiwa na Ramadhani ya pili, na akazungukiwa katika Ramadhani ya pili na siku saba ambazo alikuwa ananyonyesha (hakufunga) kwa hoja alikuwa na maradhi, na imekaribia kuingia Ramdhani ya tatu, tupeni faida, Allah awalipeni thawabu.

س19: امرأةٌ أفطرت في رمضان سبعة أيامٍ وهي نفساء، ولم تقض حتى أتاها رمضان الثاني، وطافها من رمضان الثاني سبعة أيامٍ وهي مرضعٌ، ولم تقض؛ بحجّة مرضٍ عندها، فماذا عليها وقد أوشك دخول رمضان الثالث؟ أفيدونا أثابكم الله.

الجواب

Jawabu la 1:

Ama akiwa mwanamke huyu kama alivyojieleza -kuwa yeye ni mgonjwa na wala hawezi kulipa-, basi wakati wowote akiweza kulipa basi na afunge; kwa sababu yeye ana udhuru hata kama ikija Ramadhani ya pili.

Ama ikiwa mwanamke huyu hana udhuru wowote ule, alikuwa akijifanya mgonjwa na anafanya uzembe, huyu hairuhusiwi kwake kuchelewesha kulipa Ramadhani mpaka Ramadhani ya pili.

Amesema Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikidaiwa swaumu ambayo natakiwa kulipa, basi siwezi kuilipa isipokuwa katika mwezi wa Shaaban.

Na kwa namna hiyo, ni juu ya mwanamke huyu ajitazame mwenyewe, ikiwa hana udhuru basi anapata dhambi, na juu yake kutubia kwa Allah, na apupie kulipa swaumu zilizo juu yake, ikiwa ana udhuru hakuna shida juu yake, hata kama ikichelewa mwaka au miaka miwili.

ﺟ19: إذا كانت هذه المرأة كما ذكرت عن نفسها -أنها في مرضٍ، ولا تستطيع القضاء- فإنها متى استطاعت صامته؛ لأنها معذورةٌ، حتى ولو جاء رمضان الثاني.

أما إذا كان لا عذر لها، وإنما تتعلل وتتهاون، فإنه لا يجوز لها أن تؤخّر قضاء رمضان إلى رمضان الثاني، قالت عائشة رضي الله عنها:

«كَانَ يَكُونُ عَلَيَّ الصَّوْمُ، فَمَا أَسْتَطِيعُ أَنْ أَقْضِيَهُ إِلَّا فِي شَعْبَانَ» [1].

[4] البخاري، كتاب الصوم، باب متى يقضي قضاء رمضان (1950)، ومسلم، كتاب الصيام، باب في جواز تأخير قضاء رمضان (151) (1147).

وعلى هذا، فعلى هذه المرأة أن تنظر في نفسها، إذا كان لا عذر لها فهي آثمةٌ، وعليها أن تتوب إلى الله، وأن تبادر بقضاء ما في ذمتها من الصّيام، وإن كانت معذورةً فلا حرج عليها، ولو تأخرت سنةً أو سنتين.