Skip to content
Orodha ya Sura /

الشُّورى

الشُّورى is chapter 42 of the Quran and has 53 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

53 Aya Sura Na. 42
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

حمٓ

H'a Mim .

Explanation & meanings · 1
  1. H'a Mim, A'yn Sin Qaf: Sura imeanzia kwa harufi hizi za kutamkwa kama ilivyo ada katika Sura nyingi katika Qur'ani.

عٓسٓقٓ

A'yn Sin Qaf .

Explanation & meanings · 1
  1. H'a Mim, A'yn Sin Qaf: Sura imeanzia kwa harufi hizi za kutamkwa kama ilivyo ada katika Sura nyingi katika Qur'ani.

كَذَٰلِكَ يُوحِيٓ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyo kuletea Wahyi wewe na walio kabla yako.

Explanation & meanings · 1
  1. Mfano wa yaliyomo katika Sura hii anakufunulia wewe na Mitume walio kuwa kabla yako, Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda kwa nguvu zake, ambaye amepanga kila kitu kwa pahala pake, kwa mujibu wa hikima katika vitendo vyake na mipango yake.

لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Ni vyake viliomo mbinguni, na viliomo katika ardhi. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ni vya Mwenyezi Mungu, peke yake, vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba, kuvimilika, na kuviendesha. Naye ni peke yake aliye tukuka kwa nafsi, na ukawa mkuu ufalme wake.

تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِن فَوۡقِهِنَّۚ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Mbingu, juu ya ukubwa wake na kushikamana kwake, zimekaribia kupasuka kutoka huko juu kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu, na kuathirika kwa taadhima yake na utukufu wake. Na Malaika wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila lisilo elekea naye, na humsifu kwa analo stahiki. Na humwomba Mwenyezi Mungu awasamehe watu wa duniani. Na Yeye Subhanahu ananabihisha kwamba hakika ni Mwenyezi Mungu tu, peke yake, ndiye Mwenye maghfira ya wote, na rehema iliyo kunjufu.