Skip to content
الشُّورى /

Aya 33

42 : 33

Aya 33 of الشُّورى (42 : 33). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الشُّورى Aya 53
Sura · الشُّورى
Kiswahili · Barawani
42 : 33

إِن يَشَأۡ يُسۡكِنِ ٱلرِّيحَ فَيَظۡلَلۡنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهۡرِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٍ

Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu akipenda huutuliza upepo kukawa shuwari; basi majahazi yaliyo thibiti juu ya bahari hutulia hayendi huko yendako. Hakika huko kwenda kwao na kusimama kwao kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni dalili wazi juu ya uweza wa Mwenyezi Mungu. Wanayazingatia hayo Waumini wenye kusubiri wakati wa dhiki, na wenye kushukuru wakati wa furaha.