42 : 49
لِّلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ يَهَبُ لِمَن يَشَآءُ إِنَٰثٗا وَيَهَبُ لِمَن يَشَآءُ ٱلذُّكُورَ
Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume,
Explanation & meanings · 1
- Ni wa Mwenyezi Mungu peke yake Ufalme wa mbingu na ardhi, kwa kuumba, kuudabiri, na kuusarifu. Yeye anaumba atakacho. Humtunukia amtakaye wana wa kike, na akamtunukia amtakaye wana wanaume bila ya wanawake.