Skip to content
Orodha ya Sura /

فُصِّلَت

فُصِّلَت is chapter 41 of the Quran and has 54 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

54 Aya Sura Na. 41
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

حمٓ

H'a Mim .

Explanation & meanings · 1
  1. (H'a Mim) Hizi harufi mbili katika harufi za alifbete zilio fungulia Sura hii kama ilivyo ada ya Qur'ani katika Sura nyingi, ili kuzindua watu watanabahi, na pia kuonyesha dalili ya muujiza wa Qur'ani.

تَنزِيلٞ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Kitabu hichi ni mteremsho wa namna ya peke yake, kutokana na Mneemeshaji wa neema kubwa na neema ndogo.

كِتَٰبٞ فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanao jua.

Explanation & meanings · 1
  1. Kitabu hichi ni namna ya peke yake kwa uzuri wake kwa matamshi na ibara yake ya utungaji, na kwa maana inavyo pambanua baina Haki na baat'ili, na bishara na onyo, na kuzitengeneza nafsi, na kupiga mifano, na kubainisha hukumu. Nacho kinasomwa kwa ulimi wa Kiarabu, chepesi kukifahamu kwa watu wanao jua.

بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا فَأَعۡرَضَ أَكۡثَرُهُمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ

Kitoacho khabari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii.

Explanation & meanings · 1
  1. Chenye kuwapa khabari njema Waumini wenye kutenda kuwa watapata neema iliyo andaliwa kwa ajili yao, na kuwakhofisha wanao kanusha kuwa watapata adhabu chungu iliyo andaliwa kwa ajili yao. Lakini wengi walikitupilia mbali, wala wasinafiike nacho, kama kwamba hawakusikia.

وَقَالُواْ قُلُوبُنَا فِيٓ أَكِنَّةٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ وَفِيٓ ءَاذَانِنَا وَقۡرٞ وَمِنۢ بَيۡنِنَا وَبَيۡنِكَ حِجَابٞ فَٱعۡمَلۡ إِنَّنَا عَٰمِلُونَ

Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayo tuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Na makafiri wakamwambia Mtume s.a.w.: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko vizito kwa hayo unayo tuitia yaliyo khusu Tawhidi (Upweke) wa Mwenyezi Mungu. Na masikioni mwetu mna uziwi, basi hayasikii hayo unayo tulingania. Na baina yetu na wewe lipo pazia nene linalo tuzuia kukubali hayo uliyo tuletea. Basi fanya utakalo, na sisi tunafanya tutakalo.