Skip to content
الشُّورى /

Aya 24

42 : 24
الشُّورى Aya 53
Sura · الشُّورى
Kiswahili · Barawani
42 : 24

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗاۖ فَإِن يَشَإِ ٱللَّهُ يَخۡتِمۡ عَلَىٰ قَلۡبِكَۗ وَيَمۡحُ ٱللَّهُ ٱلۡبَٰطِلَ وَيُحِقُّ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Ati wanasema: Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda atapiga muhuri juu ya moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaufuta upotofu na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliomo vifuani.

Explanation & meanings · 1
  1. Je! makafiri wanasema Muhammad anamzulia uwongo Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu akipenda atakufungia moyo wako usubiri maudhi yao, na tuhuma yao kuwa unamzulia Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ataondoa na ataushinda ukafiri na ataupa nguvu Uislamu na ataudhihirisha kwa wa'hyi alio mteremshia Mtume wake s.a.w., kwani - Yeye- Mwenyezi Mungu anajua yote yaliomo ndani ya nyoyo zenu nyote.