Skip to content
الشُّورى /

Aya 13

42 : 13

Aya 13 of الشُّورى (42 : 13). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الشُّورى Aya 53
Sura · الشُّورى
Kiswahili · Barawani
42 : 13

۞ شَرَعَ لَكُم مِّنَ ٱلدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِۦ نُوحٗا وَٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَمَا وَصَّيۡنَا بِهِۦٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰٓۖ أَنۡ أَقِيمُواْ ٱلدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُواْ فِيهِۚ كَبُرَ عَلَى ٱلۡمُشۡرِكِينَ مَا تَدۡعُوهُمۡ إِلَيۡهِۚ ٱللَّهُ يَجۡتَبِيٓ إِلَيۡهِ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِيٓ إِلَيۡهِ مَن يُنِيبُ

Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.

Explanation & meanings · 1
  1. Amekufanyieni sharia itikadi kama alivyo agana na Nuhu, na tulizo kufunulia wewe kwa Wahyi, na tulivyo agana na Ibrahim, na Musa, na Isa, ya kwamba mzitie imara nguzo za Dini, kwa kuyafuata yaliyo letwa na Dini, wala msikhitalifiane katika jambo hilo. Ni uzito kwa washirikina hayo unayo waitia ya kusimamisha nguzo za Dini. Mwenyezi Mungu humteuwa kwa ajili ya Ujumbe wake amtakaye, na humwezesha na kumsaidia katika Imani na kusimama katika Dini mwenye kuacha inda na kumwelekea Yeye.