Skip to content
Ash-Shura /

Aya 48

42 : 48

Aya 48 of Ash-Shura (42 : 48). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Ash-Shura Aya 53
Sura · Ash-Shura
Kiswahili · Barawani
42 : 48

فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظًاۖ إِنۡ عَلَيۡكَ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَإِنَّآ إِذَآ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ فَرِحَ بِهَاۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ فَإِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ كَفُورٞ

Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu. Na hakika Sisi tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyo yatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru.

Explanation & meanings · 1
  1. Wakipuuza washirikina kukuitikia wewe, ewe Mtume, basi usihuzunike. Kwani wewe si mwangalizi wao kwa hayo wanayo yatenda. Wewe umelazimishwa kufikisha Ujumbe tu, na hayo umeyabainisha wazi. Na tabia ya watu tukiwapa wasaa hupanda kiburi. Na ukiwasibu msiba kwa sababu ya maasi yao, mara wanasahau neema, wanahuzunika kwa kuteremkiwa na balaa, na wanaingia katika kufuru.