Skip to content
الشُّورى /

Aya 18

42 : 18

Aya 18 of الشُّورى (42 : 18). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الشُّورى Aya 53
Sura · الشُّورى
Kiswahili · Barawani
42 : 18

يَسۡتَعۡجِلُ بِهَا ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِهَاۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مُشۡفِقُونَ مِنۡهَا وَيَعۡلَمُونَ أَنَّهَا ٱلۡحَقُّۗ أَلَآ إِنَّ ٱلَّذِينَ يُمَارُونَ فِي ٱلسَّاعَةِ لَفِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٍ

Wasio amini huihimiza hiyo Saa ifike upesi; lakini wanao amini wanaiogopa, na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanao bishana katika khabari za hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa.

Explanation & meanings · 1
  1. Wanahimiza ije Saa ya Kiyama upesi upesi, kwa maskhara, hao wasio iamini. Na wenye kuiamini wamo katika khofu isitokee. Hao hawaihimizi. Na wanajua kuwa hiyo ni kweli iliyo thibiti, wala haina shaka. Naye Subhanahu anazindua kwamba hao wanao bisha kuja kwake bila ya shaka wamo katika upotovu ulio mbali na Haki.